MTAALAMU WA KEMIKALI WA IS AKAMATWA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 10 March 2016

MTAALAMU WA KEMIKALI WA IS AKAMATWA.

Image copyrightAP
Image captionWapiganaji wa Islamic State
Mtaalamu wa masuala ya silaha za kemikali katika wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq amekamatwa na vikosi maalum vya Marekani na sasa anahojiwa.
Mtu huyo alikuwa mtaalamu wa masuala ya silaha za kibaiolojia wa aliyekuwa rais wa Iraq Sadam Hussein ,aliyepinduliwa na uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003,duru za Iraq na zile za Marekani zimeambia vyombo vya habari vya Marekani.
Akijulikana kama Sleiman Daoud al_fari,aliripotiwa kukamatwa mwezi uliopita.
Hata hivyo,msemaji wake amesema kuwa vikosi maalum vya Marekani vimeanza oparesheni zake nchini Iraq,ikiwa ni mwanzo wa vita vikali dhidi ya Islamic State.
Mtu huyo amewaambia wanaomuhoji vile kundi la Islamic State lilivyotumia gesi ya sumu katika makombora yake,duru za Marekani zimeambia gazeti la The New York Times.
bbc swahili.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT