Mkutano ulipangwa kufanyika katika jimbo la Chicago nchini Marekani wa mgombea wa chama cha Republican Donald Trump umehairishwa baada ya kutokea maandamano.
Mkutano huo ulifutwa pia kutokana na sababu za kiusalama baada ya bwana Trump kukutana na maafisa wanaohusika na masuala ya usalama wa eneo hilo.
Mamia ya watu walikuwa wamekusanyika nje ya chuo ya Illinois saa chache kabla ya bwana Trump kuwasili.
Mapema polisi waliwakamata zaidi ya watu 30 katika mkutano wa Trump katika jimbo la Missouri.
Ndani ya ukumbi wa mkutano huo vita vilizuka kati ya wafuasi wa na waandamanaji ambao walipeperusha bendera na kutoa matamshi.
Taarifa kutoka kampeni ya bwana Trump ilisema kuwa mgombea huyo aliamua kufutilia mbali mkutano huo baada ya kukutana na maafisa wa polisi.
Katika mkutano huo kulikuwa na matamshi ya kumsifu bwana Trump kutoka kwa wafuasi wake huku baadhi ya waandamanaji wakitoa matamshi ya kumsifu Bernie Sanders.
BBC SWAHILI.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT