Muungano wa mataifa ya kiarabu Arab League umetangaza kuwa vuguvugu la kishia nchini Lebanon Hezbollah ni kundi la kigaidi,wiki moja baada ya tangazo kama hilo kutolewa na mataifa ya ghuba.
Muungano huo uliotawaliwa na mataifa yenye idadi kubwa ya waislamu wa Sunni umesema kuwa uamuzi huo uliotolewa na mataifa yote.
Hezbollah ni kundi muhimu la kisiasa pamoja na kijeshi nchini Lebanon na linahusika na vita vinavyoendelea nchini Syria.
Kwa kumuunga mkono rais Bashar al Assad kundi hilo ni adui mkubwa wa mataifa ya Ghuba yanyaowaungha mkono waasi.
Waandishi wanasema kuwa hatua hiyo ya Arab League,kufuatia hatua kama hiyo ya mataifa yanayoongozwa na Saudia itatoa shinikizo kubwa kwa kundi la Hezbollah.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT