Mashabiki wa Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa mwaka 2017 watapata nafasi ya kuona wachezaji wawili wanaotoka katika Ligi ya Tanzania wakizitumikia timu zao za taifa katika michuano ya mataifa ya Afrika 2017, michuano ambayo itafanyika Gabon.
Michuano ya AFCON itaanza kuchezwa mwakani katika nchi ya Gabon lakini mashabiki Ligi Kuu Tanzania bara watapata fursa ya kuwaona Juuko Murshid wa Simbaakiichezea Uganda The Cranes baada ya wiki hii, yeye aliichezea Uganda na kuiwezesha kufuzu AFCON kwa mara ya kwanza katika historia baada ya miaka 38.
Staa mwingine atakayeonekana AFCON 2017 ni Vincent Bossou anayeichezea Yangana timu ya taifa ya Togo, licha ya Bossou kuwa mchezaji pekee wa Ligi Kuu Tanzaniabara aliyewahi kucheza Kombe la Dunia, mwakani ataonekana tena akiichezea Togokatika michuano ya AFCON.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT