KENYA YAFANYA MCHUJO WA WAWAKILISHI WA OLIMPIKI RIO 2016. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 30 June 2016

KENYA YAFANYA MCHUJO WA WAWAKILISHI WA OLIMPIKI RIO 2016.

Mbio

Image captionMbio za wanawake mita 10,000 zimefanyika leo
Kenya imeanza kufanya mchujo wa wanariadha watakaowakilisha taifa hilo katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika mjini Rio de Janeiro, Brazil mwezi Agosti.
Shughuli hiyo inafanyika katika mji wa Eldoret, mji ambao unapatikana katika eneo ambalo ni chimbuko la wanariadha wengi bingwa.
Michezo ya Olimpiki itaanza Agosti 5 na kumalizika Agosti 21.
Kenya inafanya mchujo baada ya mtafaruku uliosababishwa na hatua ya shirika la kukabiliana na matumizi ya dawa zilizoharamishwa michezoni (Wada) kutangaza kwamba Kenya haikuwa imetimiza masharti yanayohitajika.
Jaribio la Kenya mara ya kwanza kupitisha sheria iliyohitajika na Wada haikufanikiwa.
Hatua hiyo iliibua wasiwasi kuhusu kushiriki kwa wanariadha wa Kenya katika michezo ya Rio.
Hata hivyo, Kenya iliongezewa muda na majuzi sheria hiyo ikapitishwa ingawa bado hakujatolewa uamuzi wowote na Wada.
Wanariadha wa Kenya wanaruhusiwa kushiriki ingawa watachunguzwa zaidi.
Maafisa kutoka shirika la Kenya la kukabiliana na dawa zilizoharamishwa michezoni na wenzao wa kanda (Rada) wanawapima wanariadha wanaoshiriki.
Leo, mchujo wa mbio za mita 10,000m upande wa wanawake ulifanyika.
Vivian Cheruiyot alishinda mbio hizo naye Betty Saina akamaliza wa pili.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT