Wafanyakazi katika wizara inayopambana na rushwa nchini Brazil wameshinikiza kuondolewa kwa waziri wake mpya.
Maandamano
hayo yanafuatiwa kutolewa kwa video ambayo Fabiano Silveira anatuhumiwa
kusikika akikosoa uchunguzi wa rushwa katika kampuni ya mafuta ya
serikali,Petrobras.Juma lililopita waziri wa mipango wa nchi hiyo
alilazimishwa kuachia madaraka baada ya kukumbwa na shutuma kama
hizo.Viongozi wote hao wawili walichaguliwa baada ya Rais Dilma Rousseff
alipoondolewa madarakani.Amekuwa akisisitiza kwa muda mrefu kuwa
mashitaka yaliyoundwa dhidi yake ni kwa ajili tu ya kuzuia upelelezi.BBC SWAHILI.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT