Takriban watu saba
waliuwawa siku ya Jumatatu mashariki mwa mji wa Asaba, nchini Nigeria
katika vita dhidi ya watu wa jamii ya Biafra wanaotaka kujitenga na
jeshi la taifa hilo kulingana shirika la habari la Associated Press
ripoti.
Raia 5 na polisi wawili wameuawa wakati vita hivyo
vilipoanza katika maandamano hayo ya kutaka uhuru wa watu wa Biafra,
kulingana na polisi wa jimbo la delta.Zaidi ya watu milioni wameuawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka wa 1967-1970, wakati jeshi lilipokuwa likipigana ili kuzuia mashariki mwa nchi hiyo kujitenga na kuunga jimbo linalojitengemea la Biafra.
Wanachama wa vuguvugu la jimbo la Biafra linalotaka kujitenga wameviambia vyombo vya habari kwamba idadi ya watu waliofariki ilikuwa juu ikilinganishwa na ile iliotolewa na maafisa wa polisi.
Raia wa Biafra na makundi mengine yaliyojitenga waliandamana siku ya jumatatu , siku ya ambayo walipata uhuru wao mwaka 1967
BBC SWAHILI.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT