Serikali ya Sudan
imewafurusha takriban raia 442 wa Eritrea ikiwemo wakimbizi sita
waliosajiliwa kurudi nchini mwao mwezi huu kulingana na kundi moja la
haki za kibinaadamu la Human Rights Watch.
''Sudan inawakamata na
kuwalazimisha raia wa Eritrea kurudi katika serikali yao ilio na
ukandamizaji bila kuwaruhusu wakimbizi kutafuta mahala pa
kujilinda,alisema Gerry Simpson'',mkimbizi mwandamizi anayehusika na
masuala ya utafiti katika HRW.Sudan inafaa kufanya kazi na shirika la umoja wa mataifa kuhusu Ukimbizi ili kuwalinda,badala ya kuwarudisha nyumbani ili wakumbane na unyanyasaji,aliongezea.
Sudan haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT