Polisi wa Ufaransa
wameongeza muda wa saa 24 ya kukaa kizuizini kwa mchezaji wa kimataifa
wa Ivory Coast Serge Aurier, huko Paris, ili kutoa nafasi zaidi ya
uchunguzi .
Aurier mwenye umri wa miaka 23 , ambaye huchezea timu ya Paris ya PSG anadaiwa kuwa na mabishano na polisi.Hapo awali alikuwa amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi mapema Jumatatu baada ya kisa hicho huko Paris.
Mchezaji huyo anadaiwa kumpiga polisi mmoja katika koo yake.
Kisa hicho kilitokea eneo la Champs Elysee katika majira ya asubuhi ambapo Aurier alikuwa akitoka kilabuni.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT