Jurgen Klopp
amefanikiwa kuifikisha Liverpool katika hatua ya fainali ya ligi ya
Uropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Villarreal.
Wakiwa nyuma kwa bao moja katika mchezo wa awali, Liverpool
walisawazisha matokeo baada ya Bruno Soriano kujifunga. Daniel Sturridge
aliongeza bao la pili baadaye na kuanza kuidididmiza timu hiyo kutoka
Uhispania baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Roberto Firmino.Baada ya mchezaji wa Villareal Victor Ruiz kutolewa kwa kadi nyekundu, Adam Lallana alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu usiku wa Alhamisi na kufanya mambo kuwa 3-0. Klopp ambaye alichukua timu hiyo kutoka kwa Brendan Rodgers mwezi Oktoba mwaka jana ameshaifikisha Liverpool katika fainali mbili huku ya kwanza ikiwa katika kombe la ligi ambapo walipoteza dhidi ya Manchester City. Kwa matokeo hayo watakutana katika fainali na mabingwa watetezi Sevilla mjini Basel Mei 18.
Sevilla walifika fainali kwa kuwacharaza Shakhtar Donetsk kwa matokeo ya jumla ya 5-3.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT