Waziri mpya wa maji
nchini Sudan Kusini katika serikali mpya ya umoja amedai kwamba
alifurushwa katika mkutano wa baraza la mawaziri kutokana na 'bow tie'
yake.
Mabior Garang De Mabior alichapisha picha yake katika
mtandao wa Facebook iliokuwa na maelezo yafuatayo:Nawasili nyumbani
baada ya kufurushwa na rais Salva Kiir katika kikao cha baraza la
mawaziri kwa kutovaa inavyohitajika.Aliandika:Baada ya kurudi nyumbani na kubadilisha ''bow tie'' yangu kutokana na ushauri wa makamu wa rais Riek Machar nilirudi katika kikao hicho kabla ya walinzi wa Salva Kiir kunizuia kuingia.
Bw Mabior ambaye ni mwandani wa aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar baadaye alisema hivi:Ni lazima waelewe kwamba serikali hii ya umoja haitakuwa kama ilivyokuwa awali.Mabadiliko yamekuja.
Serikali ya umoja iliapishwa wiki iliopita kulingana na makubaliano yaliolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza Disemba 2013.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT