Jumla ya wanafunzi 62 wa chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya wamefukuzwa kutoka chuo hicho, baada ya kushuhudiwa ghasia zilizosababisha kufungwa kwa chuo kwa muda usio julikana wiki moja iliyopita.
Wanafunzi waliteketeza kwa moto Ofisi za chuo hicho kutokana na kile kinachotajwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa kumchagua kiongozi wa wanafunzi chuoni.
Chuo kikuu cha Nairobi kilisema kuwa kilichukua hatua hizo za kinidhamu dhidi ya wanafunzi walioshiriki katika kuharibu mali ya umma.
bbc swahili.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT