PANYA WAILAZIMU UINGEREZA KUKODISHA PAKA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Wednesday, 13 April 2016

PANYA WAILAZIMU UINGEREZA KUKODISHA PAKA.

Image captionPanya wailazimu Uingereza kukodisha paka
Je unampenda paka ?
Awe ni paka wa nyumbani ama yule paka wa mwituni na wanyama wote katika jamii ya pakaa kama vile simba,ama chui, paka huvutia hisia nyingi sana kwa mwanadamu.
Video za paka ni maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii.
Image captionJe unampenda paka ?
Lakini mapenzi hayo ya paka yamefikia hatu mpya.
Amini usiamini ofisi ya masuala ya nchi za kigeni ya Uingereza imekodisha paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika makao makuu yake huko Westminster.
Image captionAfisi ya maswala ya nchi za kigeni ya Uingereza imekodisha paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika makao makuu yake huko Westminster.
Paka huyo ambaye zamani alinusuriwa alipokuwa akizurura mitaani katika mji mkuu wa London -- alipewa jina Palmerston, jina la waziri mashuhuri wa zamani wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza na waziri mkuu karne ya kumi na tisa.
Kituo cha kuwanusuru wanyama, kimesema kwamba Palmerston, alikuwa mkakamavu na paka mwenye nguvu, ambaye haikuwa vigumu kwake kuwa na marafiki -- au maadui, katika makao hayo yake mapya katika ofisi ya wizara ya nchi za kigeni.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT