BESIGYE AACHILIWA NA POLISI UGANDA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 18 February 2016

BESIGYE AACHILIWA NA POLISI UGANDA.


Image copyrightBBC World Service

Msemaji wa chama cha Forum for Democratic Change Ssemujju Ibrahim Nganda amethibitisha kwamba mgombea urais wa chama hicho Dkt Kizza Besigye aliyekuwa amekamatwa na polisi sasa ameachiliwa huru.
Kanali huyo mstaafu ambaye ni kigogo wa upinzani nchini Uganda alikuwa amekamatwa katika kitongoji cha Naguru, mjini Kampala katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.
Wafuasi wa upinzani, wakiambatana na kanali Besigye, wanadai walifumania watu wakiiba kura na wakataka usaidizi wa polisi kukagua nyumba hiyo lakini wakazuiliwa.
Besigye alikamatwa na maafisa wa polisi walioondoka naye kutoka eneo hilo.
Haijabainika alipelekwa wapi.
Hii na mara ya pili kwa Dkt Besigye kukamatwa wiki hii.

BesigyeImage copyrightAP
Image captionJumatatu polisi walisema walimzuilia kumlinda

Polisi walisema hakuwa na idhini ya kupitia eneo hilo kwa mujibu wa sheria.

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT