bongo satellite.: Sayansi.
Breaking News
Loading...
Showing posts with label Sayansi.. Show all posts
Showing posts with label Sayansi.. Show all posts

Tuesday, 27 September 2016

Mwezi wa Jupiter 'unatoa michirizi ya maji'.

Europa

Image copyrightNASA
Image captionMwezi wa Europa ni moja ya maeneo ambayo wanasayansi wanatafuta iwapo kuna viumbe wanaoishi anga za juu
Wanasayansi wanasema wamepata ushahidi kuwa mojawapo ya miezi inayozunguka sayari ya Jupiter imekuwa ikimwaga maji mengi anga za juu.
Wanasayansi waliripoti mara ya kwanza kuhusu kuwepo kwa maji katika mwezi huo kwa jina Europa mwaka 2013 baada ya kuufuatilia kwa karibu kwa kutumia darubini kwa jina Hubble.
Sasa, wamethibitisha hilo baada ya kuitumia Hubble kuchunguza mwezi huo ulipokuwa unapita mbele ya sayari ya Jupiter (Zohali).
Walitumia darubini hiyo kuchunguza nguvu za mionzi ya jua kuona ikiwa ilikuwa inamezwa na kitu chochote kutoka kwa mwezi huo.
Walichunguza mara kumi, na mara tatu wakafuatilia kilichoonekana kama "vidole vyeusi' vilivyokuwa vikitoka kwa Europa.
Mtaalamu aliyeongoza uchunguzi huo William Sparks, anasema hawezi kufikiria kitu kingine kinachoweza kusababisha jambo kama hilo kando na maji.
Michirizi hiyo  inayoaminika kuwa ni ya maji ilionekana eneo ambalo miaka kadha iliyopita, wanasayansi waliokuwa wakitumia Hubble, waligundua oksijeni na haidrojeni, viungo vinavyounda maji.
Ni hatua muhimu kwa sababu Europa, sehemu yake kubwa imefunikwa na bahari ya maji, na ni moja ya maeneo ambayo inaaminika huenda kukawa na viumbe wanaoishi anga za juu kando na dunia.
Wanasayansi wanakadiria kwamba huenda wakaweza kuchota maji hayo na kuyafanyia uchunguzi kwa kupitisha chombo cha anga za juu kwenye michirizi hiyo.
Njia nyingine, ambayo inausisha kupeleka chombo ambacho kitatua katika mwezi huo na kuchimba kilomita nyingi ndani ya barafu ili kufikia maji, huenda ikawa na changamoto nyingi sana.
EuropaImage copyrightNASA/ESA/W. SPARKS (STSCI)/USGS
Image captionMichirizi ya maji ambayo ilionekana katika mwezi kwa jina Europa
EuropaImage copyrightNASA
Image captionMichoro kwenye sehemu ya juu ya mwezi wa Europa, ambao umefunikwa pakubwa na barafu
Michirizi ya maji imewahi kuonekana katika mwezi wa Enceladus, mwezi wenye barafu wa sayari ya Saturn (Sarteni).
Chombo cha anga za juu cha Cassini kwa sasa kinazunguka sayari hiyo na tayari kimepitia katika michirizi hiyo kufanya uchunguzi.
Hata hivyo, vifaa vya chombo hicho havina uwezo wa kuchunguza uwepo wa viumbe hai.
bbc.

Tuesday, 30 August 2016

Tanzania kupata ugeni wa watalii duniani kushuhudia kupatwa kwa jua.

Kupatwa kwa jua  au Annular Eclipse hutokea pale jua na mwezi zinapokuwa kwenye mstari mmoja ambapo umbo la mwezi linaonekana kuwa dogo zaidi kuliko umbo la jua.
Wanayansi wanasema kwamba September 1, 2016 Tanzania ndio itakuwa sehemu pekee ambayo kupatwa huko kwa jua kutaonekana vyema na kuwavutia watalii wengi.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya Uingereza imeripoti kwamba kupatwa huko kwa jua kutaanza kwenye bahari ya Altantic, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Msumbiji, kisiwa cha Madagascar kisha kwenye Bahari ya Hindi.
tanzania-eclipse-phil-hart
Wataalamu wanasema kwamba miongoni mwa maeneo yatakayoonekana vizuri kwa kupatwa kwa jua ni Mbeya na Tunduru, Ruvuma ambapo tukio hilo litachukua dakika 3 hadi dakika 7.
Millard Ayo.

.

Wednesday, 10 August 2016

Wanasayansi wamethibitisha kwamba kunguru mwitu wanaweza kutemgeneza zana.

Kunguru mwitu

Image copyrightRUTZ GROUP
Image captionKunguru mwitu wanaweza kutengeneza zana
Wanasayansi wamethibitisha kwamba aina ya kunguru mwitu kutoka New Caledonia kusini mwa Pacific wanaweza kutengeneza zana.
Ndege hao walichunguzwa walipokua wakitumia midomo yao kuchukora chakula kilichokua kimefichwa kati kati ya mbao.
Awali ujuzi huu ullibainika kwa ndege wanaotunza kwenye maabara .
matokeo ya uchunguzi uliochapishwa kwenye jarida la Open Science, yanasema kuwa kipaji hiki ni sehemu ya tabia asilia ya ndege.
Mwaka 2002, kunguru mwitu anaetunzwa kwenye maabara ya New Caledonian crow - kwa jina Betty - aliwashangaza wanasayansi.
Watafiti katika chuo kikuu cha Oxford walimpatia chakula katika kikapu kisichoweza kufikiwa kwa urahisi.
Kukifikia , ndege huyo alipindisha kipande cha waya hadi ndani ya kikapu. Ilikua ni mara ya kwanza kwa ujuzi huo wa kutengeneza kifaa kuwahi kushuhudiwa katika ulimwengu wa wanyama.
Betty alikufa mwaka 2005, lakini baada ya miaka, hatimae uchunguzi ulifanikiwa kurudiwa katika ndege mwingine alieko kwenye maabara.
Mkuu wa uchunguzi huo Dr Christian Rutz, kutoka chuo kikuu cha St Andrews cha Scotland, anasema : "ilionekana ni kama ni kitu ambacho ndege yule alikivumbua katika maabara ."
Wakati inafahamika kwa muda mrefu kwamba kunguru wa porini huweza kudonoa vitu kutoka kwenye sehemu zilizojificha za ndani , watafiti sasa wamebaini kuwa wanaweza pia kupindisha vijiti sawsa na wenzao wa maabara.
Kunguru mwituImage copyrightRUTZ GROUP
Image captionKunguru 10 kati ya 18 waliweza kutengeneza vijiti vya kudonolea chakula
Katika msururu wa uchunguzi , watafiti waliwakamata kunguru kutoka misitu ya New Caledonia, na kuwaweka kwa muda mfupi katika viota vya muda
Dr Rutz anasema: "Hii inamaanisha kwamba tunaweza kuwafanyia majaribio katika hali ya uchunguzi unaodhibitiwa zaidi - lakini aina za vipimo tunavyofanya pale, havionyeshi vema namna ndege hawa walivuyo na akili , wanauliza ni aina gani ya kifaa ambacho wanakielezea kwa tabia asilia.
Kunguru walipewa vijiti , ambavyo vilikua na ladha ya chakula ambavyo viliwekwa kwenye mashimo kwenye sakafu
"Kitu kimoja tu tulichowapatia ulikua ni mmea ambao tulifahamu kwa kawaida wanatumia kutengenezea kifaa mwituni ," alieleza Dr Rutz.
"kwa hiyo kazi ilikua rahisi sana , tuliomnba ndege wetu watengeneze vifaa kisha tuvitumie kutoa chakula kilichofichwa ."
Kunguru hawakuhitaji vijiti maridadi kuchukua chakula , lakini 10 kati ya 18 wa mwituni walifanya hivyo.