PICHA 12: Daraja la kioo China lasitishwa kutumika baada ya siku 13. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Saturday, 3 September 2016

PICHA 12: Daraja la kioo China lasitishwa kutumika baada ya siku 13.


Daraja la kioo ambalo limeelezwa kuwa liko juu zaidi liliziduliwa hivi karibuni nchini China ambapo lina urefu wa zaidi ya futi 1400, upana wa futi 20 na karibu futi 1000 kutoka kwenye ardhi na imeripotiwa kuwa kioo chake ni imara zaidi mara 25 zaidi ya kioo cha dirisha.
Daraja hilo la wapita kwa miguu lijulikanalo kwa jina la daraja la Zhangjiajie lilizinduliwa August 20 mwaka huu ambapo lina uwezo wa kuchukua watu hadi 800 kwa wakati mmoja. Imeelezwa kuwa daraja hilo limekuwa likitumika kwa shughuli mbalimbali za kiutalii.
Daraja hilo limelazimika kufungwa ili kufanyiwa maboresho ya ndani baada ya idadi kubwa ya watalii waliokusanyika kutembelea kweye daraja hilo. Daraja hilo ambalo liko Kusini mwa China liligharimu dola million 48 kujengwa, na lilifunguliwa August 20 na limesitishwa huduma zake leo.
Msemaji wa kivutio hicho aliiambia MailOnline kuwa daraja lilitengenezwa ili kuweza kuchukua kiwango cha juu cha watu ambao ni 800 kwa wakati mmoja, na limepokea takribani watu 10,000 ambao ni watalii tangu lifunguliwe, msemaji huyo alisisitiza kuwa ni sehemu ya kioo ya daraja ni salama. 
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
Millard Ayo.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT