Licha ya kufungwa na Nigeria gavana katoa zawadi ya dola kwa Taifa Stars. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Monday, 5 September 2016

Licha ya kufungwa na Nigeria gavana katoa zawadi ya dola kwa Taifa Stars.


September 3 2016 ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilicheza mchezo wake wa mwisho wa kuwania kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2017 na timu taifa ya Nigeria katika uwanja wa Uyo uliyopo katika jimbo la Akwa Ibom State.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kukamilisha ratiba kwa timu zote mbili Taifa Stars walifungwa goli 1-0 goli ambalo lilifungwa na nyota wa Man City Kelechi Iheanacho dakika ya 77 ya mchezo baada ya kupiga shuti lililomshinda golikipa wa Tanzania Aishi Manula, licha ya kufungwa Taifa Stars walionesha uwezo mkubwa wa kupambana kiasi cha gavana wa jimbo hilo kuwapa zawadi.
Gavana wa jimbo la Akwa Ibom State alitoa zawadi ya dola 10,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 21 kwa wachezaji wa Taifa Stars kutokana na uwezo waliouonesha, fedha hizo walipewa katika hafla ya chakula cha pamoja baada ya mchezo huo.
CHANZO: Shaffihdauda

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT