Serikali ya Sudan Kusini inasema kuwa zaidi ya watu 40 wameuawa kwenye mapigano ya hivi majuzi katika mji wa Wau na kuongeza kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Waziri wa habari Michael Makuei, anasema kuwa maiti za raia 39 zimepatikana na pia za polisi wanne.
Kulikuwa na mapigano makubwa ndani na nje ya mji wa Wau ulio kaskazini mwa nchi siku ya Jumamosi.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini alisema kuwa vikosi vyake vilipigana na makundi yaliyokuwa yamejihami pamoja na wale waliowataja kuwa wapiganaji wa makabila.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT