TANZANIA:ALIYEMDHIHAKI RAIS MAGUFULI AHUKUMIWA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 9 June 2016

TANZANIA:ALIYEMDHIHAKI RAIS MAGUFULI AHUKUMIWA.

Image copyrightSTATEHOUSE TANZANIA
Image captionRais Magufuli
Mtu aliyemdhihaki rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amehukumiwa na mahakama ya Tanzania.
Kulingana na mtandao wa EATV5, Mtuhumiwa huyo Isack Habakuki alipigwa faini ya shilingi milioni 7 na hakimu mkazi wa Arusha Augustine Rwizile.
Hababuki alipatikana na kosa la kumuita bwege Rais John Pombe Magufuli kupitia mtandao wa kijamii.
Akisoma hukumu hiyo katika mahakama ya Arusha,hakimu huyo alisema kwamba kwa kuwa kosa hilo lilikuwa la kwanza mbali na kutetewa vikali na wakili wake mahakama iliamua mshtakiwa apunguziwe adhabu.
Vievile Kulingana na mtandao huo,simu yake aliyotumia kutuma ujumbe huo wa kuudhi katika mitandao ya kijamii imetaifishwa.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa wakili wa serikali, Vitalisi Timoni, aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa huyo aliandika ujumbe huo mnamo mwezi Machi 17 mwaka huu na walipofanya utafiti walimtambua kabla ya kumkamatwa na kuhojiwa katika kituo cha Polisi Osterbei Dar es Salaam ambapo alikiri kuandika ujumbe huo.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT