Sarafu ya Nigeria imeanza kuuzwa katika soko la hisa ambapo thamani yake itakuwa ikitegemea mahitaji yake, kinyume na ilivyokuwa hapo awali ambapo benki kuu ilikuwa imeweka kiwango cha ubadilishanaji.
Kutokana na hatua hiyo thamani ya naira ilishuka mara moja kwa asilimia 23.
Muda mfupi baada ya kuanza kwa biashara leo Jumatatu, thamani ya naira ilikuwa ni naira 255 kwa dola moja ya Marekani.
Thamani ambayo ilikuwepo awali ilikuwa ni naira 197 kwa dola.
Wachanganuzi wanasema kuwa kushuka kwa bei ya mafuta, imesababisha thamani ya naira kushuka.
Bei ya naira katika masoko yasiyo halali ni 350 kwa dola moja ya Marekani.
bbc,
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT