MLIPUKO WA BOMU WAWAUA WATU 18 SOMALIA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 30 June 2016

MLIPUKO WA BOMU WAWAUA WATU 18 SOMALIA.


Image copyrightEPA
Image captionMlipuko wa bomu Somalia

Habari kutoka Somalia zinasema kuwa watu 18 wameuawa baada ya bomu kulipuka na kuharibu kabisa basi walimokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba abiria. Wote waliouawa walikuwa raia.
Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa karibu wa Lafole.
Inadhaniwa kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi lililokuwa karibu.
Mara kwa mara wapiganaji wa Al Shaabab hulenga wanajeshi wa Serikali.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT