MICHEZO:UBELGIJI YAILAZA JAMHURI YA IRELAND. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Saturday, 18 June 2016

MICHEZO:UBELGIJI YAILAZA JAMHURI YA IRELAND.

Image copyrightAFP
Image captionWitsel wa Ubelgiji akisheherekea bao lake
Romelu Lukaku alifunga mabao mawili huku timu ya taifa la Ubelgiji ikipata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Euro2016 na kuharibu fursa ya timu ya Jamhuri ya Ireland kufika robo fainali.
Baada ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza ambapo hakuna timu ilioona lango la mwengine,Lukaku aliifungia Ubelgiji bao la kwanza baada ya kupata pasi muruwa.
Image copyrightAP
Image captionUbelgiji
Baadaye Axel Witsel alifunga bao la pili kupitia kichwa katika dakika ya 61,kabla ya Lukaku kufunga bao la tatu baada ya kushambulia ngome ya Ireland.
Image copyrightREUTERS
Image captionLukaku
Timu ya Jamhuri ya Ireland ilishindwa kufanya mashambulio katika ngome ya Ubelgiji.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT