Aliyekuwa makamu wa rais wa Maldives, amehukumiwa kifungo cha miaka kumi na mitano gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kupanga njama ya kumuua rais wa nchi hiyo.
Bwana Ahmed Adeed, alipatikana na hatia ya kuhusika na shambulio la bomu, ambalo lililipua boti ya rais Abdulla Yameen mwaka uliopita.
Mapema wiki hii, Bwana Adeeb alihukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani kwa kumiliki silaha.
Yeye ni afisa wa ngazi ya juu zaidi kufungwa kwa tuhuma za ugaidi tangu bwana Yameen alipochaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo mwaka wa 2013.
Wapinzani wakuu wa rais wa nchi hiyo wako gerezani au wanaishi uhamishoni.
Mawakili wa bwana Adeeb wamesema kuwa watakata rufaa ya hukumu hiyo.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT