Shirika la kutetea haki za kibinadam la Amnesty International, limetoa taarifa likiishutumu vikali serikali ya Nigeria, kwa kuhusika na mauaji ya watu wa kabila la Biafra ambao hawakuwa wamejihami.
Katika ripoti iliyotumwwa kwa vyombo vya habari, shirika hilo limedai watu arubaini waliuawa na wengine hamsini kujeruhiwa wakati wanachama wa kundi moja linalotaja eneo hilo kujitenga walipokuwa wakifanya sherehe mjini Onitsha, Kusini Mashariki mwa Nigeria mwezi uliopita.
Shirika la Amnesty international limetoa wito kwa serikali ya Nigeria kuanzisha uchunguzi kufuatia kuawa kwa raia wengi wa kabila ndogo ka Biafra ambao hawakuwa wamejihami, na kuwafungulia mashtaka waliohusika na uhalifu huo.
Shirika hilo limesema limekusanya ushahidi kuthibitisha kuwa wanajeshi wa Nigeria waliwafyatulia risasi wafuasi wa wa kundi linalotaka eneo la Biafra kujitenga IPOB na wapita njia wengine mjini Onista.
Aidha limesema uchunguzi wao wa awali umebainisha kuwa watu kumi na saba waliuawa na wengine hamsini kujeruhiwa.
Shirika hilo limesema wengi wa waliouawa au kujeruhiwa wangali wanazuiliwa na jeshi na polisi.
Mkwa mujibu wa Amnesty International, wanajeshi wa nchi hiyo waliwafyatulia risasi wafuasi wa IPOB waliokuwa wakiandamana Agosti mwaka uliopita watika uhuru wa jimbo hilo la Biafra.
Hata hivyo jeshi la Nigeria limekanusha madai hayo kupitia naibu msemaji wake Kanali HA GAMBO.
Kanali Gambo amesema ripoti hiyo haina msingi wowote na kudai kwua eneo hilo lilikuwa linakabiliwa na tishio la kutekwa na wanamgambo wa kiislamu.
bbc.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT