UHABA MKUBWA WA MAFUTA BURUNDI. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Friday, 6 May 2016

UHABA MKUBWA WA MAFUTA BURUNDI.


Image copyright THINKSTOCK Image caption Waziri wa nishati hata hivyo anasema nchi hiyo ina mafuta ya kutosha
Uhaba mkubwa wa mafuta umeshuhudiwa katika mji mkuu wa Bujumbura na maeneo mengine nchini Burundi.
Kwa karibu wiki moja sasa, vituo vya kuuza mafuta vimekabiliwa na uhaba mkubwa na wateja wanalazimika kupanga foleni kwenye vituo ambavyo bado havijamaliza mafuta.
Waziri wa nishati nchini humo aliambia runinga ya taifa Alhamisi kwamba hakuna sababu yoyote ya kuvifanya vituo vya mafuta kukosa mafuta ya kuuza.
Alisema taifa hilo bado lina mafuta ya kutosheleza mahitaji.
Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Prime Ndikumagenge anasema licha ya hakikisho la waziri, uhaba bado umeendelea kushuhudiwa.
Baadhi ya watu wanasema huenda wanunuzi wa mafuta kwa wingi wameshindwa kupata fedha za kigeni za kutosha kuagiza petroli kutoka nje.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT