MAMBO 10 YA AJABU YALIYOZIDI LEICESTER KUSHINDA EPL.
Image copyright
Klabu ya Leicester City
imeshinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza. Mwanzo wa msimu Agosti mwaka jana uwezekano wao kushinda ligi ulikuwa umekadiriwa kuwa 5,000/1.
Miezi minane baadaye, ndio mabingwa.
Kwa
mujibu wa kampuni ya uwekaji dau ya William Hill, uwezekano wa
Leicester kushinda ligi ulikuwa sawa na wa Scott Mills kushinda tuzo ya
Oscar. Lakini kuna mambo mengine ya kushangaza zaidi ambao uwezekano
wake kutokea ulikuwa juu. Haya hapa mambo kumi ya kushangaza:
1. Simon Cowell kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza - 500/1
Image copyrightAPImage caption
Simon Cowell na Mwanamfalme Charles
Uwezekano wa Jaji wa kipindi cha televisheni
cha X Factor Simon Cowell kuwa waziri mkuu Uingereza ulikuwa mara 10 juu
ya uwezekano wa Leicester kushinda taji, katika kampuni ya uwekaji dau
ya Ladbrokes.
2. Piers Morgan kuwa meneja wa Arsenal - 2,500/1
Image copyrightGetty ImagesMorgan kwa sasa ni mtangazaji wa kipindi cha Good
Morning Britain katika runinga ya ITV. Agosti mwaka jana, uwezekano wake
kuingia kwenye soka na kuwa mkufunzi wa Arsenal ulikuwa juu kuliko
Leicester kushinda ligi.
3. Sir Alex Ferguson kushinda Strictly Come Dancing - 1,000/1
August 2015, Ladbrokes walikuwa na dau ya meneja wa
muda mrefu wa Manchester United Sir Alex Ferguson kushinda Strictly
Come Dancing katika 1,000/1.
4. Malkia Elizabeth kuchomoa wimbo wa Krismasi - 1,000/1
Malkia Elizabeth kwa sasa ana umri wa miaka
90, lakini kunao waliodhani angeweza kutoa kibao ambacho kingeongoza
katika tasnia ya muziki Krismasi kuliko Leicester kushinda ligi msimu wa
2015/16.
5. Jitu la Loch Ness kupatikana - 500/1
Wengi waliamini picha hii iliashiria uwepo wa
jitu kwa jina Loch Ness na mwaka jana Paddy Power walikuwa na dau ya
500/1 ya uwezekano wa jitu hilo kupatikana.
Kulikuwa na habari
zaidi mwaka huu kuhusu loch, kwani ilibainika picha hiyo ilitoka kwa
mfano wa Loch Ness ulioundwa mwaka 1969 kutumiwa katika filamu ya
Sherlock Holmes.
6. Kate na William kujaliwa pacha watatu- 1,000/1
Bintimfalme Charlotte alisherehekea mwaka
mmoja tangu kuzaliwa lakini katika Paddy Power dau ya Kate na William
kupata pacha watatu ilikuwa na uwezekano wa 1,000/1 Agosti mwaka jana.
7. Dean Gaffney kupata tuzo ya Oscar - 1,000/1
Dean Gaffney alijiondoa kipindi cha
EastEnders mwaka 2003, lakini Paddy Power walikuwa na dau ya 1,000/1 ya
Gaffney kushinda tuzo ya Oscar ya mwigizaji bora.
8. Kim Kardashian kuwa rais Marekani - 2,000/1
Image copyrightGetty ImagesMumewe, Kanye West, tayari ametangaza
atawania urais 2020, lakini kunao walioamini Kim anaweza pia kuwania.
Uwezekano wa hilo kutokea katika Paddy Power ulikuwa 2,000/1.
9. Elvis Presley yuko hai? - 2,000/1
Dau ya uwezekano wa mwanamuziki Elvis
Presley, aliyefariki 1977, kupatikana akiwa hai na buheri wa afya 2016
ilikuwa na uwezekano wa juu kutokea badala ya Leicester City kushinda
Ligi ya Premia.
Paddy Power waliweka nafasi hiyo kuwa 2,000/1.
10. Grimmy kushinda Olimpiki?
Kampuni ya uwekaji dau ya William Hill iliweka
uwezekano wa dj wa redioni Radio 1 Nick Grimshaw kushinda dhahabu
Michezo ya Olimpiki ya Rio katika kiwango sawa s - 5,000/1 - na
Leicester City kushinda ligi ya EPL.
0 comments:
POST A COMMENT