MAPIGANO BADO YAENDELEA YEMEN. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Tuesday, 12 April 2016

MAPIGANO BADO YAENDELEA YEMEN.

Image copyright
Image captionZaidi ya watu 6000 wameuwawa kutokana na vita nchini Yemen.
Kumekuwa na mapingano ya hapa na pale nchini Yemen wakati wa siku pili ya kutekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha vita yanayoongozwa na umoja wa mataifa.
Viongozi wamesema wanajeshi wa Rais Abedrabbo Mansour Hadi, walipambana na wanamgambo wa Houthi katika mkoa wa Marib , karibu na mji unaodhibitiwa na waasi wa Sanaa.
Image copyrightReuters
Image captionShambulizi mjini Sanaa
Kwingineko mshambuliaji wa kujitolea mhanga amejilipua karibu na uwanja wa soka kusini mwa bandari ya Aden na kuwauwa watu wanne.
Watu wengine 10 wamejeruhiwa katika shambulio hilo, ambalo lilikuwa limelenga wanajeshi walioajiriwa.
Zaidi ya watu 6000 wameuwawa kutokana na vita nchini Yemen.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT