Wodi tatu za wagonjwa katika hospitali ya Leicester Royal nchini Uingereza zimefungwa baada ya wagonjwa 16 wa saratani kupatikana na homa ya nguruwe.
Wagonjwa hao wanaougua virusi hivyo vya H1N1 wanatibiwa katika hospitali ya Glenfield iliopo mjini humo.
Madaktari wamewataka wale wanaougua ishara za homa kukaa mbali na eneo hilo.
''Wagonjwa 16 katika wodi tatu za hospitali hiyo ya Leicester wameanza kuwa na ishara ambazo zimethibitishwa kuwa zile za homa''.
''Hatua zote za tahadhari zimechukuliwa na wagonjwa hawa wametengwa ili kuzuia mlipuko,''hospitali hiyo imesema.
Wagonjwa hao 3, katika hospitali ya Glenfield wanapokea matibabu ya watu wanaougua ugonjwa wa moyo au matatizo ya mapafu.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT