Serikali ya Syria na kundi la wapinzani zimesema kuwa zinakubali mpango wa kusitisha uhasama kati yao kuanzia jumamosi.
Serikali imesema itasitisha mapigano ya kijeshi sambamba na mpango uliotangazwa na serikali za Marekani na Urusi.
Lakini upinzani umesema kuwa makubaliano hayo yatategemea majeshi ya serikali kusitisha mashambulizi dhidi ya raia.
Mpango huo hatahivyo hautayahusisha makundi mawili ya jihad nchini Syria ikiwemo Islamic State na kundi la al-Nusra Front.
Al-Nusra Front lina uhusiano na kundi la al-Qaeda na ni kundi kubwa la muungano wa wapiganaji.
Umoja wa mataifa umekiri kwamba utekelezaji wa mpango huo utakumbwa na chagamoto si haba.
Zaidi ya raia 250,000 wamefariki katika kipindi cha miaka mitano ya vita nchini Syria.
Watu wengine milioni 11 wametoroka makwao huku vikosi vinavyomtii rais Bashar al Asaad na wale wanaopinga uongozi wake vikikabiliana pamoja na wapiganaji wa kiislamu.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT