Habari hizi zinasambaa katika mitandao ya kijamii baada ya video iliyotumwa katika ukurasa wa Instagram kuonyesha wanafunzi wakivutana na askari shuleni kwao.
Video hiyo iliyotumwa katika ukurasa huo inamuonyesha msichana wa miaka 13, Zulaikha Patel na wanafunzi wenzake, wakikabiliana na askari wa ulinzi, huku wakiwa wamenyoosha mikono juu “tuchukueni sisi wote…”
Wanafunzi hao walisema waliamua kuandamana baada ya kuambiwa kwa kejeli na waalimu wao kwamba nywele zao sio za asili na zinahitajika kufugwa kama mnyama.
“Suala la nywele zangu limekuwa ni jambo lililoniandama maisha yangu yote, tangu nikiwa shule ya msingi nilikuwa nikiambiwa nywele zangu sio za asili, ni za kubandika, afro langu halikuhitajika kabisa, suala hili limeniandama mpaka shule ya sekondari sasa”. Alisema mwanafunzi wa shule ya Pretoria, Patel.
Aidha kanuni za maadili katika shule ya wasichana ya Pretoria hazijaonyesha ufugaji wa afro, lakini ina sheria zinazojumuisha muonekano wote wa mwanafunzi ikijumuisha aina zote za nywele zinatakiwa kuwa safi na kuendana na sare ya shule.

Zulaikha Patel
Shule ya Pretoria ilianzishwa mwaka 1902, ikiwa na wanafunzi weupe tupu, lakini tangu mwaka 1990 ilibadilishwa na kuwa ya watu wote. Hivyo wengi wanahisi kwamba tukio hili linahusisha mambo ya ubaguzi wa rangi unao endelea nchini kwao.
Wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kuonesha watu kwamba ni kwa vipi suala hili bado linaendela licha ya kuwa taifa hilo limkuwa katika demokrasia iluyoharamisha ubaguzi kwa miaka 22 sasa.
“Tukiwa shuleni tunajifunza majina yetu ni magumu, pua zetu ni mbaya, nywele zetu ni mbaya, ngozi zetu ni chafu. #achaubaguzishuleni August 28, 2016” waliandika kwenye ukurasa wa Instagram
“Inaniuma sana…kila wakati Napata huzuni ninapoona kijana wa Afrika Kusini anafanyiwa ubaguzi” waliandika kwenye ukurasa wa Instagram.

Katika taarifa ya hivi karibuni, idara ya elimu ya jimbo la Gauteng imesema kwamba, baada ya kuitembelea shule hiyo Waziri wa elimu wa jimbo hilo, Panyaza Lesufi, ametaka kufanyika kikao na kutazama upya sheria na kanuni za maadili za shule hiyo.
“Kanuni za Maadili ya shule lazima kupitiwa upya na kukifanyia kazi kifungu hicho cha nywele, kwa sasa kifungu hicho kisimamishwe kwa muda”. Alisema Waziri wa Elimu Panyaza.
LAUDANUS MAJANI (UDSM-SJMC)
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT