Gondwe akamata malori usiku. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Saturday, 10 September 2016

Gondwe akamata malori usiku.



Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe 

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe  
Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe amekamata malori saba yakisafirisha madini ya chuma aina  dolomiteyanayotumika kutengeneza saruji.
Gondwe amesema kati ya  malori saba walifanikiwa kukamata matano, huku mawili madereva wakiwahi kutoroka. “Malori hayo yalikuwa yanatokea Kata ya Mgambo, yanakochimbwa madini hayo,” amesema.
Kufuatia hatua hiyo, Gondwe ametangaza kupiga marufuku usafirishaji  madini usiku.
“Tulipokamata magari hayo, kwanza tuliwauliza kama wamelipa kodi na kama wamelipa watuonyeshe stakabadhi,” amesema.
Alisema madini yanapo safirishwa nje ya wilaya mfanyabiashara anatakiwa kuilipa Serikali Kuu asilimia tatu na halmashauri inatakiwa kulipwa asilimia 0.3 ya mauzo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, William Makufwe amesema wamekuwa wakipoteza mapato kupitia wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi.
Makufwe amesema  wameanza kukusanya  kodi  kwa kutumia wataalamu wao na kuachana na mawakala, ambao walikuwa wanawasilisha fedha kidogo.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilaya za Handeni na Kilindi, Charles Kamuhanda alisema kumekuwa na changamoto ya ulipaji kodi kutoka kwa wafanyabiashara. 
Mwananchi.

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT