3 wapigwa risasi na kuuawa Burlington Marekani. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Saturday, 24 September 2016

3 wapigwa risasi na kuuawa Burlington Marekani.

Maduka ya Cascade Mall Burlington Marekani

Image copyrightAP
Polisi katika jimbo la Washington nchini Marekani wanasema kuwa watu watatu wamepigwa risasi na kufariki na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
Wanasema shambulio hilo lilitokea katika eneo la Burlington, mwendo wa saa moja hivi kutoka mji wa Seattle.
Shambulio hilo lilitekelezwa Ijumaa alasiri katika maduka ya Cascade Mall.
Awali polisi walisema kuwa ni watu wanne waliokuwa wameuawa kwa kupigwa risasi lakini kwa sasa wameeleza kuwa wanawake watatu walipatikana wameuawa katika maduka ya Macy na mwanamume mmoja amepelekwa hospitalini akiwa na majeraha mabaya.
Polisi wamechapisha picha hii ya mshukiwaImage copyrightAP
Image captionPolisi wamechapisha picha hii ya mshukiwa
Ilichukua muda wa saa kadhaa kabla ya eneo hilo kutangazwa kuwa salama tena kabla ya wauguzi kuruhusiwa kuingia ndani kuwahudumia watu waliokuwa wamejeruhiwa.
Polisi wamechapisha picha ya mshukiwa huyo wa kipekee ambaye wamemtaja kuwa mwenye asili ya Uhispania, aliyeonekana akibeba bunduki.
Kulingana na polisi alionekana mara ya mwisho akitembelea kuelekea kwenye barabara kuu.
Watu katika eneo hilo wameshauriwa wasalie ndani ya nyumba zao na wafunge milango.
bbc.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT