Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na URA katikia mchezo wa wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Taifa.
Kwenye mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Taifa, dar es Salaam, wageni walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 19 kupitia kwa Bokota Labama aliyefunga kwa kichwa.
Simba, ambayo ilitumia mchezo huo kumuaga nahodha wake, Mussa Hassan Mgosi aliyeamua kustaafu soka na kupewa umeneja wa timu hiyo, walisawazisha dakika ya 31 kupitia kwa kiungo Jonas Mkude aliyeunganisha mkwaju wa adhabu wa Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Mchezo huo ni wa mwisho kwa kocha Joseph Omog wa Simba kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wikiendi ijayo.
Mchezo huo maalumu kwa kumuaga Mgosi ulionekana kuwa tofauti na ule wa awali wa Simba Day dhidi ya FC Leopards ya Kenya, ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0. Mgosi alitua tena Simba akitokea Mtibwa alipokuwa na msimu mzuri, lakini aliishia kufunga bao moja msimu uliopita.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT