Mfalme akihito wa Japan aomba kung'atuka. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Monday, 8 August 2016

Mfalme akihito wa Japan aomba kung'atuka.

Mfalme Akihito

Image copyrightREUTERS
Image captionWananchi waonekana kushangaa baada ya Mfalme Akihito kutangaza matamanio yake ya kung'atuka
Mfalme wa Japan Akihito ameeleza mapenzi yake ya kutaka kung'atuka.
Akihutubia taifa hilo kupitia runinga, amesema ana wasiwasi kwamba umri na udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.
Kwa sasa, hakuna nafasi kisheria kumruhusu mfalme kuondoka madarakani Japan.
Lakini muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema atathmini kwa makini matamanio ya mfalme huyo.
Mfalme AkihitoImage copyrightNHK
Image captionMfalme Akihito
Mfalme Akihito amekuwa madarakani tangu kifo cha babake, Hirohito, mwaka 1989.
Habari kwamba anataka kung'atuka zilianza kutokea kwenye vyombo vya habari mwezi jana.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT