Serikali imefuta usajili wa Magazeti 473 kupitia tangazo lililochapishwa katika gazeti la serikali lenye namba 195. Sababu za kufutwa usajili wa magazeti 473 ni kutokana na magazeti hayo kutochapishwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.
Magazeti hayo hayataruhusiwa kuchapishwa au kusambazwa kwa njia ya nakala ngumu au kielektroniki, ikiwa Mmiliki wa gazeti lililofutiwa usajili angependa kuendelea na biashara milango iko wazi kwa ajili ya kuwasilisha maombi mapya ya usajili kwa kufuata taratibu zilizopo.
Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya msajili wa magazeti Tanzania inayo magazeti na majarida 881 yaliyosajiliwa kisheria.
millard ayo.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT