Mkoa wa Morogoro umebaini kuwapo kwa watumishi hewa 315 waliolipwa zaidi ya Sh2 bilioni baada ya kufanya uhakiki upya huku Wilaya ya Kilosa ikiwa kinara.
Awali mkoa huo, ulibainika kuwa na watumishi hewa 122 katika halmashauri zake zote za wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe amesema baada ya kupokea taarifa hizo hakuridhishwa na kuamua kuunda timu ya watu saba kuhakiki zaidi.
Amesema Kilosa imeongoza kwa kubainika kuwa na watumishi hewa 98 ikifuatiwa na Kilombero 48, Ulanga 44, Mvomero 20, Gairo 13, Morogoro 38, Malinyi saba na ofisi ya mkuu wa mkoa na hospitali ya rufaa ya mkoa watano.
chanzo: Mwananchi
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT