WATU 50 WAFARIKI KATIKA AJALI GHANA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 18 February 2016

WATU 50 WAFARIKI KATIKA AJALI GHANA.


Image captionRais wa Ghana John Mahama
Takriban watu 50 wamefariki katika ajali mbaya ya barabarani kuwahi kufanyika nchini Ghana katika kipindi cha miaka mingi.
Basi moja lililokuwa limejaa abiria liligongana ana kwa ana na lori lililojaa tomato kaskazini mwa taifa hilo siku ya jumatano jioni.
Rais wa Ghana John Mahama ameielezea ajali hiyo kama ''habari mbaya'' katika mtandao wake wa tweeter na kuongezea kuwa huduma ya kukabiliana na maswala ya dharura inakabiliana na hali hiyo.
Baadhi ya walionusurika wamewaambia polisi kwamba breki za lori hilo zilifeli ,lakini kiini cha ajali hiyo kinachunguzwa.
Hatahivyo kuna hasira na shutma katika mitandao ya kijamii baada ya picha za kuogofya za ajali hiyo kusambazwa.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT