SHAMBULIO LA HOSPITALI NI UHALIFU WA KIVITA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Tuesday, 16 February 2016

SHAMBULIO LA HOSPITALI NI UHALIFU WA KIVITA.


Image copyright
Image captionHospitali ya Syria ilioshambuliwa
Ufaransa na Uturuki zimesema kuwa mashambulio ya angani yaliolenga hospitali Kaskazini mwa Syria yanashirikisha uhalifu wa kivita.
Hadi watu 50 wameuawa katika mashambulio katika hospitali na shule katika jimbo hilo,kulingana na umoja wa Mataifa.
Wizara ya masuala ya kigeni nchini Uturuki imelaumu Urusi kwa shambulio hilo.Moscow hatahivyo haijatoa tamko lake kuhusu madai hayo.
Image copyrightepa
Image captionhospitali
Wakati huohuo rais wa Syria Bashar al Assad ana wasiwasi kuhusu mpango wa kusitisha vita nchini Syria.
Wiki iliopita mataifa yenye uwezo mkubwa duniani yalikubaliana kushirikiana kupitia makubaliano ya amani ,ambayo yataanza baadaye wiki hii.
Lakini katika matamshi yake kuhusu tangazo hilo,Rais Assad alisema kuwa usitishwaji huo wa vita haumaanishi kwamba pande zote zitaweka chini silaha zao.
Image copyrightAFP
Image captionmashambulio ya Syria
''Kwa sasa wanasema kuwa wanataka vita visitishwe kwa juma moja'',alisema katika runinga.''Ni nani anayeweza kufuatilia masharti haya yote na mahitaji yake kwa juma moja''?.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa misururu ya mashambulizi kaskazini mwa Syria inatilia shaka kuhusu masharti hayo ya kusitisha vita.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT