Bunge la Haiti limemchagua rais wa mpito, juma moja baada ya aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Michel Martelly, kuondoka madarakani, na hivyo kuacha nchi bila ya uongozi.
Kiongozi mpya, Jocelerme Privert, alichaguliwa baada ya kikao kirefu cha bunge, ambacho kiliendelea hadi leo alfajiri.
Bwana Privert ni kiongozi wa sasa wa bunge.
Ataongoza nchi kwa kipindi kisichozidi miezi minne, wakati Haiti inatarajiwa kufanya uchaguzi mwingine wa rais.
Duru ya pili ya uchaguzi wa rais ilivunjwa mwezi uliopita, kwa sababu ya ghasia na tuhuma za udanganyifu.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT