MSHAMBULIZI AWAUWA WATU 6 SAUDIA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 11 February 2016

MSHAMBULIZI AWAUWA WATU 6 SAUDIA.


Image captionSaudia

Mshambuliaji amefyatua risasi katika ofisi ya idara moja ya elimu nchini Saudia, kusini mwa mkoa wa Jazan,na kuwauwa wafanyakazi wengine sita ,maafisa wamesema.
Watu wengine wawili walijeruhiwa katika shambulio hilo,lililofanyika katika jamii ya mashambani ya Ad Dair,karibu na mpaka na Yemen.
Mshambuliaji huyo amekamatwa ,afisa mmoja amesema.
Hakuna sababu ya shambulio hilo iliotolewa,na mamlaka inasema kuwa inalichukulia swala hilo kama la uhalifu.
Mshukiwa huyo hajajulikana lakini, kituo cha habari cha AFP,kikinukuu runinga ya Al-Ekhbariya ,imeripoti kwamba mtu huyo hakuwa mfanyakazi lakini alikuwa na biashara katika wizara hiyo.
Ripoti za awali zilisema kuwa mshambuliaji huyo alikuwa mwalimu.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT