Mkewe waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu ,Sara aliwatusi na kuwatendea maovu wafanyakazi wake wa nyumbani ,mahakama moja ya wafanyakazi imebaini katika kesi iliowasilishwa na aliyekuwa msimamizi wa nyumba hiyo.
Mahakama hiyo ilikubali madai ya Meni Naftali kwamba alitusiwa vibaya na baadaye kumlipa dola 43,000 kama fidia.
Uamuzi huo umesema kuwa hasira za Bi. Netanyahu ziliathiri mazingira ya wafanyakazi wake.
Bi. Netanyahu alisema kuwa madai hayo yalikuwa ya uongo akisema kuwa ana uhusiano mzuri na wafanyakazi.
Afisi ya waziri mkuu haikutoa tamko lolote kuhusu uamuzi huo.Ilikana madai ya hapo mbeleni dhidi ya Bi Netanyahu kama maovu na ya kusengenya.
Kesi ya awali ambapo alituhumiwa kwa kumtusi muuzaji duka mmoja ilitatuliwa nje ya mahakama.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT