WEST HAM YAITUPA NJE LIVERPOOL. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 11 February 2016

WEST HAM YAITUPA NJE LIVERPOOL.


Image copyrightGetty
Image captionRaha ya mechi bao, wachezaji wa West Ham United wakishangilia
Wagonga nyundo wa London West Ham United imewatupa nje majogoo wa Anfield Liverpool katika mchezo wa raundi ya nne ya kombe la FA.
West Ham walianza kuandika bao lao la kwanza kupitia kwa Michail Antonio katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza baada ya kunganisha krosi nzuri Enner Valencia's
Liverpool wakachomoa bao hilo kupitia kwa kiungo Philippe Coutinho aliyepiga mpira wa adhabu na kujaa nyavuni moja kwa moja.
West HamImage copyrightGetty
Image captionWest Ham sasa watakutana na Blackburn raundi ijayo
Dakika tisini zikamalizika kwa sare ya bao 1-1, katika dakika 30, za nyongeza West Ham wakapata bao kupita kwa Angelo Ogbonna,
West Ham watawavaa Blackburn ugenini katika mchezo wa raundi ya tano ya michuano hiyo hapo Februari 21.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT