NDOVU AINGIA MJINI NA KUHANGAISHA WATU INDIA. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 11 February 2016

NDOVU AINGIA MJINI NA KUHANGAISHA WATU INDIA.


Ndovu mwitu aliingia katika mji mmoja katika jimbo la Bengal Magharibi nchini India na kuhangaisha wakazi kwa saa kadha.
Maafisa walitumia vishale vyenye dawa ya kutuliza wanyama kumtuliza.
NdovuImage copyrightEPA
Image captionNdovu huyo aliharibu nyumba na magari
Lakini tayari alikuwa ameharibu nyumba, magari na pikipiki kabla ya kudhibitiwa.
Hata hivyo, maafisa wa mji huo wa Siliguri wanasema hakuna mtu aliyeumizwa wakati wa kisa hicho.
NdovuImage copyrightAP
Image captionWatu waliojawa na wasiwasi walikimbia kumkwepa
Ndovu huyo baadaye alipelekwa kwenye hifadhi moja ya wanyama ambayo hutumiwa kuwafuga ndovu na wanasema wanapanga kumrejesha porini baadaye.
Watu walioshuhudia wanasema ndovu huyo aliingia mjini kutoka msitu ulio karibu na alionekana kuwa na wasiwasi na kukanganyikiwa.
Kisa hicho kimetokea siku chache tu baada ya chui kuingia shuleni na kujeruhi watu sita katika eneo la Bengaluru.
VishaleImage copyrightReuters
Image captionMaafisa walitumia vishale vyenye dawa kumtuliza
NdovuImage copyrightAP
Image captionWalioshuhudia wanasema ndovu huyo alionekana kuwa na wasiwasi
NdovuImage copyrightReuters
Image captionMaafisa walitumia kreni kumuinua na kumuingiza kwenye lori baada ya kumtuliza
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT