JESHI LA KENYA LAMUUA KAMANDA WA AL-SHABAB. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 18 February 2016

JESHI LA KENYA LAMUUA KAMANDA WA AL-SHABAB.


Image copyrightAP
Image captionWanajeshi wa Kenya nchini Somalia

Jeshi la Kenya KDF limethibitisha kuwa limemuua kiongozi wa al-shabab anayesimamia intelijensia ya kundi hilo Mohammed Karatey pamoja na makamanda wengine 10.
KDF limesema kuwa liliwaua wapiganaji hao katika shambulio kubwa  mnamo tarehe 8 mwezi Februari.
Kulingana na taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na wizara ya Ulinzi nchini Kenya,wapiganaji hao waliuawa katika kambi ya Nadaris kati ya Buale na Sukow.

Image copyrightd
Image captionwapiganaji wa al-shabab

Inadaiwa kuwa Karatey alikuwa amezuru kambi hiyo kwa hafla ya kufuzu kwa takriban wapiganaji 80 wapya wa alamnyat waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi.Inadaiwa kuwa wapiganaji 42 waliuawa huku wengine wengi wakipata majeraha.
Kitengo cha alamnyat ndicho chenye wapiganaji wa kujitolea muhanga,wataalamu wa vilipuzi na watafutaji habari hivyobasi mauji ya kamanda huyo ni pigo kubwa wa alshabab.

Image captionNdege ya wanajeshi wa Kenya

Inaaminika kuwa Karatey alikuwa na jukumu kubwa katika uvamizi wa kambi ya jeshi la Kenya huko El Ade ambapo aliwatumia walipuaji wake.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT