NENO LA MUNGU LINA UJASIRI,SOMA HAPA KUJUA NI VIPI UTAWEZA KUDAI KUTOFARIKI CHINI YA MUDA ALIOSEMA MUNGU. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 7 April 2016

NENO LA MUNGU LINA UJASIRI,SOMA HAPA KUJUA NI VIPI UTAWEZA KUDAI KUTOFARIKI CHINI YA MUDA ALIOSEMA MUNGU.

TAFADHALI SOMA HATA MWISHO NI MUHIMU ZAIDI YA MAMBO YA ULIMWENGU HUU UNAYOYAPA MASAA MENGI KWENYE MUDA WAKO,NINAKUSIHI: BWANA YESU KRISTO ASIFIWE MPENDWA,HABARI ZA WAKATI HUU, Ninapenda nikushirikishe jambo hili ambalo Roho Wa Mungu amekuwa akinishuhudia siku nyingi,ila msukumo ulizidi hasa leo nilipokuwa katika maombi ya alfajiri,na naona sasa nimepewa kibali cha kukiandika nikiongozwa na Roho Mtakatifu. Na baada ya kusoma haya natumai mabadiliko ndani mwako ya kuishi kimazoea bila kuhoji yatafanyika. JE MUNGU ANAZUNGUMZIAJE SUALA LA KIFO,JUU YA MWANADAMU?JE YEYE NDIYE MSABABISHI WA KILA KIFO KINACHOTOKEA?JE HATUWEZI KUTATHMINI MATATIZO YA VIFO KUWA YANASABABISHWA NA NINI?NA KUACHA LAWAMA JUU YA MUNGU? Vifo vingi(Mauti kuwakumba wanadamu)vimekuwa vikitokea kutokana na sababu mbalimbali,lakini imekuwa vyepesi sana mwanadamu kuelekeza lawama kwa Mungu kuwa Yeye ndiye kampenda zaidi,kwamba mwanadamu huyo apumzishwe mahala pema peponi alimaarufu kwa Lugha ya Kiingereza kama R.I.P(Kwa maana ya Rest In Peace).Pia imekuwa rahisi sana mwanadamu kutomsifu Mungu na kumtukuza amtendeapo Matendo Makuu ila wakati apato matatizo huelekeza lawama kwa Mungu. Swali langu kuu ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa sisi wanadamu kusema Mungu kampenda zaidi yetu ni hili,Mungu anamchukua yule mtu ili akamfanyie nini,(Ninao hoji ni walio chini ya Umri uliotajwa kwenye BIBLIA),Kwa maana nikiangalia mwingine ni mtoto,hajawatumikia hata wazazi wake licha ya Mungu,nikiangalia mwingine ni kijana hajamtumikia hata Mungu maana maneno ya Mungu yasema hivi; MHUBIRI 12:1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo. Na nikiangalia wengine ni wazee ambao bado wako chini ya umri ambao Mungu anawatambua kuwa bado ni watoto chini ya miaka 100. Kipindi cha Wana wa Israeli ghadhabu ya Mungu ilikuwa juu sana na Musa mtumishi wa Mungu alipata kazi sana kuhojiana na Mungu ili atulize yale ambayo aliyadhamiria juu ya Wana wa Israeli ambao pamoja na matendo makuu ya Mungu walioshuhudia kwa macho yao walizidi kukengeuka sana hasa katika kuabudu sanamu na miungu iliyomuudhi Mungu sana,Mungu bado alizikubali sadaka zao za Amani,na aliwarehemu kwa rehema Zake zilizo nyingi,aliwaua pia kwa hasira na ghahabu yake kutokana na ukaidi wao juu ya Amri na Sheria za Mungu,hapo tuliona kweli Mungu akiwaangamiza watu wake kwaajili ya machukizo yao,pia hata wakati wa Nuhu. Katika kizazi chetu ni kwamba tunayo Neema Kubwa ya YESU KRISTO damu yake yenye thamani iliyomwagika msalabani ilishatupatanisha na Mungu,na hutupatanisha katika kutubu kwetu,mawazo,maneno,na matendo pia ya kila siku(Onyo sio kukusudia kutenda dhambi kisa kuna kusamehewa,la hasha bali ni katika kutimiza lile la kuwa tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,soma (WARUMI 3:23).Tu hekalu la Mungu,maana Mungu Baba,Mungu Mwana na Roho Mtakatifu wako nawe,je ataligeukia hekalu lake kuliangamiza kama sio mtenda dhambi? Ninachosukumwa kuandika ni hiki maana Mungu amechukizwa na kusingiziwa kwake vifo vya watoto wake,vifo vya umri wa miaka chini ya 70,80,100,120 sio mpango wa Mungu na neno kumpenda Yeye zaidi yetu lisitumike tena maana Yeye sio muaji ni Mungu wa wote wenye mwili soma YEREMIA 32:27,jihoji anawapeleka wapi hao anaosemwa kuwauwa Yeye?je utakuwa sahihi kumtupia Mungu lawama?tuangalie BIBLIA na Mungu mwenyewe anasemaje,tatizo kubwa limejikita hapa Kuangamizwa kwa kukosa marifa,tunauliwa na Mapepo,Majini,Mawakala wa shetani,Wachawi,Waganga wa kienyeji kwenye ufalme wa giza,mamlaka ya giza,wakuu wa giza,mapepo ya majeshi wabaya WAEFESO 6:12,ndio wanaotuangamiza kabla ya wakati wa Mungu na tumefungwa akili ya kutotambua ili tusipambane nao,ili wazidi kupata damu na nyama ya kumlishia shetani,hii inatokea kwenye ajali za ndege,magari,meli,wakati wa kuvuka barabara,hospitalini,kukaliwa na ugonjwa wa muda mrefu,vifo vya ghafla visivyo na sababu,wakati wa kujifungua kina mama,kuharibika mimba,kujiuwa,kunywa pombe,kutumia madawa ya kulevya,nk na pia hatutaki kujiunganisha na Mungu asilimia mia katika kuzifuata amri na sheria zake,tamaa zetu za mwili shetani anatuteka nazo hadi kutuuwa,kwa nini kifo kitokee wakati hujui?una mamlaka ya kuzuia lolote lile ukiwa umejikabidhi kwa Mungu,ikiwa umemkiri Yesu Kristo kuwa ni BWANA na mwokozi wa maisha yako,Yeye,Na Baba yake watashuka na kuweka makao ndani mwako,wakati Yeye amesema hivi kwenye AMOSI 3:7. Hakika BWANA MUNGU hatafanya neno lolote,bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.Ukijiunganisha na Mungu asilimia mia hakuna jambo litakalotokea kwa kushtukiza. HOSEA 4:6. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;tunukuu hadi hapo,ufalme wa giza ndio unaosababisha vifo vyote chini ya wakati wa Mungu. ZABURI 90:10. Siku za miaka yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;(niishie hapo katika kunukuu ili uone Miaka halali ya wewe kudai kutoka kwa Muumba wako utoke katika giza uingie katika nuru,ni Daudi alizungumza hivyo,tuangalie MUNGU mwenyewe anasemaje ISAYA 65:20. Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache,wala mzee asiyetimia siku zake;kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia;bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa. Kumbe dhambi zetu tamaa zetu ambazo tunashawishiwa,tunatekwa na kuuliwa na shetani ndizo zitutiazo mautini,bali watakaoishi katika utakatifu wa Mungu kwa kuzishika amri zake na kuzitenda sheria hata katika kipindi hiki cha neema umri wao ndio huu umetajwa hapo juu na hata wakati wa Mungu ukifika utajuzwa,sio huu wa kufa tu kwa vifo chini ya wakati wa Mungu. MWANZO 6:3. BWANA akasema,Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele,kwa kuwa yeye naye ni nyama;basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Je katika huu uchambuzi na rejea za KIBIBLIA bado una haki ya kusema Mungu kampenda zaidi yetu mtu anayefariki chini ya umri aliosema Mungu?amkeni tupambane na ufalme wa giza unao shawishi kwa dhambi watu,unaoteka,unaouwa ili kula nyama na kunywa damu,maana wana hasira wakijuwa wakati wao utawadia ambao jiwe halitasalia juu ya jingine,mwingine anaweza akaibua swali,kwanini Mungu aruhusu shetani atuangamize wakati tu watoto wake?ni hivi tunaangamizwa kwa kukosa maarifa na hatuyataki,shetani imeandikwa kabisa ni mshtaki wetu kila sekunde mbele za Mungu kumbuka Yeye awali kabla ya kuasi alikuwa malaika mkuu na anajua Neno,hivyo kama huna Neno la kupingana naye ndani mwako,jua ataruhusiwa kukuletea na mauti .Hapa sio kukariri mistari,bali kujaza Neno ndani mwako kwa kusoma MWANZO HADI UFUNUO,kwa kuyatafuta maarifa ya Mungu na ufalme wake kwanza. Juu ya suala la kulazwa mahala pema peponi hizo ni njia tu za kufarijiana wanadamu,ila ukweli ni kwamba kama mtu kafia dhambi hakuna mwanadamu wa kubadilisha hukumu ya Mungu juu yake hata tufunge miaka 1000 maana Yeye ni wa kutenda hukumu za haki,wakati wa kutubu na kukubalika kuandikwa katika kitabu cha uzima ni wakati wa wewe kuwa hai wala si vyinginevyo,maana hakuna mtumishi wa Mungu atakaye simama kuwaombea watu wafu rehema akakubalika,ukifia kwenye dhambi ni hukumu na kisha baadaye kuunguzwa pamoja na shetani,ukifa katika utakatifu ni uzima wa milele utakuwa na Mungu mwenyewe. KATAA KIFO KABLA YA WAKATI WA MUNGU ULIODHIBITISHWA,KATAA KWA WATOTO,MUME WAKO,MKE WAKO,KIJANA BINTI NA KIJANA MVULANA KATAA,MPINGE Shetani naye atakukimbia,wala Roho ya Mauti haitatafuna tena familia yako,MUNGU ANASEMA ATALIANGALIA NENO LAKE ILI ALITIMIZE YEREMIA 1:12,ATALIANGALIA HATA KATIKA WEWE KUFIKIA UMRI SAHIHI ENDAPO WEWE UMEMKUBALI YEYE NA KUMKATAA Shetani bila aibu. NATUMAI UMEPATA WAKATI SAHIHI WA WEWE KUONDOKA KATIKA ULIMWENGU HUU. Ninamshukuru Mungu Baba,Mungu Mwana na Roho Mtakatifu kwa kunipaa wasaa mzuri na nguvu,ujasiri wa kuandika haya,na sasa najiskia mwepesi baada ya kulitua jambo hili kwa Watoto wake ili maarifa yaongezeke na wawe wanahoji masuala mbalimbali kwenye ulimwengu huu. Niishie hapa,na inuka sasa jivalishe silaha zake Mungu mpinge shetani naye atakukimbia,pinga utafunaji wake wa kusababisha vifo na kuwauwa watu wako kabla ya wakati wa Mungu hasa nyote kujiunganisha kwake Mungu ili upate haki yako. Nimeandika mimi mwenyewe kwa mikono yangu kwa uwezo wake Roho Mtakatifu. UBARIKIWE,MAOMBI YANGU NI WEWE KUTAFUTA MAARIFA YA MUNGU ILI UMWEZE Shetani. @ Gideon Kiyyian Ole Kiyiapi
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT