Klabu za Uingereza za Manchester City na Liverpool zitafahamu wapinzani wao katika nusu fainali michuano ya Ulaya leo.
Droo ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya itafanywa saa sita unusu mchana saa za Afrika Mashariki.
City, ambao msimu ujao watakuwa chini ya Pep Guardiola, huenda wakakabidhiwa klabu yake ya sasa Bayern Munich kutoka Ujerumani.
Klabu hizo nyingine zilizo kwenye droo ni Atletico Madrid na Real Madrid kutoka Uhispania.
Droo ya Europa League itafanyika saa moja baadaye, klabu zilizo kwenye droo zikiwa Liverpool, Sevilla, Shakhtar Donetsk na Villarreal.
Liverpool walifika nusufainali kwa kulaza Borussia Dortmund Alhamisi kwenye mechi ya kusisimua wakitoka nyuma 2-0 wakati wa mapumziko na kushinda 4-3 uwanjani Anfield.
Walifanikisha ushindi wa jumla wa 5-4.
Sevilla, ambao wanapigania kushinda kikombe kwa mara ya tatu mtawalia, walitinga nusufainali kwa kuwashinda Athletic Bilbao kupitia mikwaju ya penalti.
![City](http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2016/04/06/160406210129_manchester_city_640x360_getty.jpg)
Bayern walifika nusufainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kuwaondoa Benfica nao City wakawatoa Paris St-Germain.
Atletico Madrid waliwaondoa mabingwa watetezi Barcelona na Real Madrid wakawaondoa Wolfsburg.
Ni mara ya kwanza kwa City kufika nusu fainali.
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT