CLINTON APUUZILIA MBALI MADAI KWAMBA HAFAI. | bongo satellite.
Breaking News
Loading...

Thursday, 7 April 2016

CLINTON APUUZILIA MBALI MADAI KWAMBA HAFAI.

Image copyrightReuters
Image captionBernie Sanders na Hillary Clinton
Mgombea wa urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Demokrat amepuuzilia mbali madai ya mgombea mwenza katika chama hicho Bernie Sanders kwamba hafai kuwa rais huku wasiwasi ukipanda katika kinyang'nyiro cha chama hicho.
Seneta huyo wa Vermon alisimama na matamashi yake ya kumuhusisha Hillary Clinton kufuatia hatua yake ya kuunga mkono vita nchini Iraq.
Anasema kuwa ni Hillary aliyeanza kumshambulia kwa maneno.
Wagombea hao wawili watakabiliana huko New York katika kipindi cha wiki mbili,jimbo ambalo wagombea wote wawili huenda wakajipatia kura nyingi.
Bwana sanders alimshinda Bi Hillary Clinton katika mchujo wa Wisconsin siku ya Jumanne,na huenda akapata wajumbe zaidi huko Wyoming siku ya Jumamosi kabla ya kinyanganyiro kikali kitakachokuwepo huko New York.
BBC SWAHILI.
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT